Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo January 11, 2018 imetoa hukumu katika kesi inayowakabili wafanyabiashara wawili wa Visiwani Zanzibar ambapo wamewahukumiwa miaka 3 jela ama kulipa faini ya Sh.Milioni 6 Naushad Suleiman (63) na Ali Makame (36) waliokiri kukamatwa wakisafirisha vipande saba vya madini ya dhahabu vyenye thamani ya Sh.milion 989.7 na fedha za nchi 15.
Pia Mahakama hiyo imeyataifisha madini hayo na fedha hizo zilizokuwa zimewekwa katika mabegi mawili kuwa mali ya serikali.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo aliwatia hatiani washtakiwa baada ya kukiri makosa yao ya kula njama na kusafirisha madini ya dhahabu vipande 7 vyenye thamani ya Sh.Milioni 989 bila leseni.
Hakimu Mashauri amesema kuwa amefikiria kwa umakini maombi ya washtakiwa hao ya kutaka kupunguziwa adhabu kwa sababu ni wakosaji wa kwanza, pia mshtakiwa Naushad ni mgonjwa wa moyo pamoja na kukiri kosa na kujutia walichokifanya.
“Ili iwe fundisho kwa watu wengine, katika kosa la kwanza mahakama inawahukumu kulipa faini ya Sh.milioni 2 ama jela miaka 2, pia kosa la pili faini Sh.mil 4 ama jela miaka 3, mkishindwa mtaenda jela na kutumikia vifungo hivyo sambamba,”– Hakimu Mashauri
Pia kuhusu dhahabu na fedha za nchi 15 walizokamatwa nazo washtakiwa, Mashauri amesema zinataifishwa na kuwa mali ya serikali. Hata hivyo, wafanyabiashara hao wamelipa faini na kuepuka kifungo hicho.
MAHAKAMANI: Maagizo waliyopewa TAKUKURU kuhusu kesi ya Malinzi
Aveva ana tatizo la figo, ashindwa kufika Mahakamani