Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro Stanley Hotay amesema Rais John Magufuli anavyotumbua watumishi na kuagiza viongozi wa serikali kupinga rushwa ni halali kabisa.
Ametoa wito pia kwa viongozi wote kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na rushwa nchini.
Pia ametoa wito kwa wafugaji wa mifugo mingi kuitumia katika kuwekeza kwenye maeneo yenye faida zaidi. Amewashauri wanaofuga ng’ombe wengi wawauze na kufanya uwekezaji katika maeneo mengine huku wakibakiwa na ng’ombe wachache wanaoweza kuwahudumia.
“Tanzania tunakimbilia uchumi wa kati, wito wangu kwa wafugaji wenye ng’ombe wengi hakikisheni mnawatumia kwa faida, kuliko kuwaacha wafe wabadilisheni kuwa uchumi mwingine.” – Stanley Hotay
Mwili wa Mke wa Kingunge ulivyoagwa nyumbani kwake leo