Kadri siku zinavyozidi kwenda Teknolojia nayo inakuwa kwa kasi leo nikupe stori kuhusu Kampuni mbili zimetengeneza pampu ambazo zitawasaidia wanawake wanaonyonyesha kukamua maziwa na kuyahifadhi wakati wakiwa safarini na kutumika pale mtoto atakapohitaji.
Wanawake wanaotumia pampu hizo kawaida hukamua maziwa mara kwa mara kwa siku na kuwapa watoto wanapokuwa wanahitaji. Kwa kawaida huunganishwa kwa umeme na hutoa sauti.
Kampuni za Willow na Freemie Libert zimetengeneza pampu hizo kwa njia ambazo zitakuwa rahisi kuvaliwa. Kinyume na za zamani, zasasa hutumia betri na hazina sauti.
Willow ilishinda tuzo kutokana na kifaa hicho kwenye maonyesho ya CES mwaka 2017, kwa sababu pampu hiyo imekuwepo kwa majaribio lakini sasa inaingia rasmi sokoni kwa shilingi milioni moja ya Kitanzania.