Tumeshuhudia baadhi ya nchi Afrika zikiwa katika mchakato wa kubadili Katiba zao ili Rais aweze kukaa madarakani kwa muda mrefu. Leo January 12, 2018 Wabunge wamebadilisha Katiba na kuondoa ukomo wa mihula kwa rais nchini Gabon tofauti na ilivyokuwa awali ambapo Rais alikaa madarakani kwa mihula miwili, kila muhula miaka saba.
Jumatano ya January 10, 2018 Bunge lilipitisha muswada wa Sheria hiyo ambayo kwa sasa inapelekwa Mahakama ya Katiba ili ipitishwe nchini Gabon.
Kupitishwa kwa sheria hii kutamfanya Rais wa sasa Ali Bongo kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi kama atachaguliwa na raia wa nchi hiyo na
Rais Bongo ataendelea kukaa madarakani kwa muda wa miaka saba, lakini pia hawezi kufunguliwa mashtaka hata baada ya kuondoka madarakani.
Upinzani umepinga mabadiliko hayo, ambayo wamesema yanalenga kumsaidia rais Bongo kuendelea kuwa madarakani.
Hali hii inashuhudiwa katika baadhi nchini Afrika kama Uganda, Burundi na nchi nyingine barani Afrika.
VIDEO: LOWASSA NA VIONGOZI WENGINE WALIVYOUAGA MWILI WA MKE WA KINGUNGE
“LOWASSA HUKU USIJE HATUKUTAKI, UKIJA UNAPUMZIKA” MUSUKUMA