Leo January 14, 2018 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Khamis Kigwangalla kwa kushirikiana na Wizara nyingine wamefanya ukaguzi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) ili kubaini changamoto za utendaji kazi wa uwanja huo.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Dk. Kigwangalla amesema kuwa ziara hiyo imehusisha Manaibu Waziri wanne, wakiongozwa na yeye Kigwangalla pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigullu Nchemba.
Dk. Kigwangallah amesema kuwa ameshuhudia idadi ya wageni inaongezeka, huku kero za kusubiri huduma za ukaguzi zikipungua.
“Zamani abiria alikuwa anachukua zaidi ya saa tatu ili akaguliwe huku akisimama sehemu ambayo ina joto, lakini sasa hivi kero zimepungua,”-Dr. Kigwangalla
Naye Waziri Mwigullu amesema idadi ya wageni wa utalii na wanaokuja kuwekeza imeongezeka nchini hivyo watajitahidi kuboresha huduma.
Pia Mwigullu amesema mbali ya kuboresha huduma hiyo, pia wataboresha huduma ya Passport na Visa kutoka kwenye mfumo wa zamani na kuwa wa kisasa wa Kieletroniki.
“Wizara tupo katika hatua ya kuhama kutoka Passport ya kawaida kwenda kwenye Passport ya kimtandao ambapo hadi kwenye Visa, mchakato huo sio wa siku moja Bali tutaongeza na idadi ya watumishi”– Dr. Mwigullu
HD VIDEO: WALICHOKUBALIANA JPM NA KAGAME KUKITIMIZA NDANI YA MWAKA HUU