Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye aliongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamis Kigwangalla pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Dr. Mwigullu Nchemba, January 14, 2018 katika ziara iliyofanyika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere ili kujionea jinsi huduma zinavyoendeshwa.
Akiongea na Waandishi wa Habari Eng. Nditiye amesema wapo katika mkakati wa upanuzi wa sehemu ya kufikia wageni na watasaini mkataba wiki ijayo.
“Suala la wageni wanapofikia tumepiga hatua kubwa sana tutasaini mkataba wiki ijayo, sehemu fulani itaanza kubomolewa kwa ajili ya kupanua eneo la wageni kufikia, lakini pia tunaongeza kaunta mbili kwa upande wa Uhamiaji kwa ajili ya kuhudumia watu kwa haraka,”– Eng. Atashasta Nditiye
GOOD NEWS: TANZANIA KUZINDUA PASSPORT ZA KIELEKTRONIKI