Leo January 16, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amepokea hati za utambulisho za Mabolozi 6 ambao wameteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi hao ni pamoja na Balozi wa Nigeria nchini Sahabu Isah Gada, Balozi wa Poland nchini Krzysztof Buzalsky, Balozi wa Uturuki Ali Davotouglu, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier.
Wengine ni Balozi wa Israel nchini Noah Gal Gandler pamoja na Balozi wa Australia nchini Alison Chatres.
Katika shughuli hii Rais Magufuli amewaahidi mabalozi hao kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wa kiuchumi uliopo kati ya Tanzania na nchi hizo pia amewasisitiza wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo kuwekeza nchini.
Ametaja maeneo makubwa ya uwekezaji nchini kuwa ni pamoja na Kilimo, Viwanda, Utalii na utoaji huduma mbalimbali za kijamii.
Watu 7 kizimbani kwa kujiunganishia bomba la mafuta ya Dizeli
Dr Tulia baada ya kusikia changamoto za watu wake Mbeya