Leo January 16, 2018 Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ameongea na waandishi wa habari na kuelezea matukio mbalimbali yaliyotokea ndani ya Jiji la DSM na kuonyesha silaha walizozikamata.
Katika taarifa yake Kamanda Mambosasa amesema kuwa kuna baadhi wahalifu waliopata msamaha wa Rais Magufuli na wamekwenda kufukua silaha walizoficha ardhini na wanazitumia kwa matukio ya uhalifu.
“Taarifa tulizonazo baada ya wahalifu wengine walioachiwa kwa msamaha wa Rais, wachache ambao hawataki kubadili tabia zao, wamekwenda kufichua silaha ambazo walizika ardhini na sasa wanaziibua na kuanza kuzitumia”.– Kamanda Mambosasa
VIDEO: ‘NI KWELI TUMEPOKEA MALALAMIKO YA MREMA NA TUNAENDELEA NA UPELELEZI’ KAMANDA MAMBOSASA