Huko nchini Uingereza kwa mara ya kwanza kwenye historia ameteuliwa Waziri wa Upweke ambaye atashughulikia na kukabiliana na tatizo hilo la upweke ambalo limeathiri mamilioni wa watu nchini humo.
Waziri huyo Tracey Crouch anatarajiwa kukabiliana na upweke ambao kwa wingi zaidi unaathiri wazee, waliopoteza wapendwa wao, wasio na watu wa kuzungumza nao na wengineo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu, takribani watu milioni tisa ni wahanga wa tatizo hilo la upweke kati ya watu milioni 65 ambao ndiyo idadi ya watu wote nchini humo.
MWANZO MWISHO: Kingunge asimulia alivyong’atwa na mbwa wake
Ilivyoendelea kesi ya Mhasibu wa TAKUKURU anayedaiwa kumiliki mali za Bilioni 3