Bayern Munich wamesisitiza hawana mpango wa kumuza kiungo wao Toni Kroos kabla ya mkataba wake kuisha mnamo mwaka 2015.
CEO wa Bayern CEO Karl-Heinz Rummenigge alisema mwezi uliopita kwamba klabu yake imeshindwa kukubaliana na mchezaji juu ya mkataba mpya kutokana na masuala ya kifedha, huku ripoti kadhaa zikisema kwamba kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani anataka alipwe mara mbili ya anavyolipwa sasa.
Manchester United wamekuwa wakihusishwa na kumsajili Kroos baada ya kocha David Moyes kuonekana akizungumza na wakala wa Kroos katika mchezo wa hivi karibuni wa Bayern, na kocha Pep Guardiola nae alichangia kuongezeka kwa tetesi hizo baada ya kusema mchezaji huyo mwenye miaka 24 anaweza kuuzwa.
Mashaka kuhusu hatma ya Kroos ndani ya klabu yaliongezeka wakati alipotolewa katika mchezo dhidi ya Stuttgart na kurusha ‘gloves’ zake kwenye benchi kwa hasira.
Hata hivyo, mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Matthias Sammer amesema kwamba klabu yake haipo tayari kumruhusu kiungo huyo kuondoka wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa wakati wa kiangazi.
“Hatuna dhamira yoyote ya kumuuza Toni hivi karibuni,” aliiambia Sueddeutsche Zeitung. “Kama Raisi Uli Hoeness alivyosema hivi karibuni: Bayern ni klabu inayonunua, sio ya kuuza.”