Leo January 20, 2018 Siku chache zilizopita Rais Kagame wa Rwanda alifanya ziara ya kikazi nchini na kuzungumza na President JPM juu ya ujenzi wa reli ya umeme, sasa GOOD NEWS ni kwamba Mawaziri watatu wa Tanzania na mmoja kutoka nchini Rwanda wamesaini mikataba ya awali kuhusu ujenzi wa reli ya umeme kutoka Isaka Tanzania mpaka Kigali nchini Rwanda.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema makubaliano hayo yanatokana na maagizo yaliyotolewa na Rais John Magufuli na Paul Kagame wa Rwanda baada ya kukutana January 14, 2018.
“Treni itakayopita katika reli hiyo itakuwa ni ya umeme, ambapo itakuwa kwa treni ya abiria itatembea speed ya Kilometre 160 kwa saa na treni ya mizigo itakuwa na speed ya Kilometre 120 kwa saa,”.– Prof. Mbarawa
Prof. Mbarawa amesema kutokana na ujenzi wa reli nyingine hasa ya kati itarahisisha usafiri ambapo kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda inaweza ikachukua saa 12 badala ya siku 2.
BREAKING: ‘NINAWAPA WIKI MOJA LA SIVYO TUTAVUNJA MKATABA NA TBA’- WAZIRI NDALICHAKO