Leo January 23, 2018 Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Butiama mkoani Mara Solomon Kamlule Ngiliule baada ya kushindwa kutimiza majukumu yake.
Hayo yamewasilishwa na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ambaye ameeleza kuwa Rais Magufuli amefikia muamuzi huo baada ya baadhi ya watendaji wa tawala hizo za mikoa na serikali za mitaa kujihushisha na ubadhirifu na kutotimiza majukumu yao.
Waziri Jafo pia amemuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuchukua hatua stahiki kwa Mtunza Hazina wa Halmahsuari hiyo aliyekuwepo wakati ubadhirifu huo ulipokuwa ukifanyika. Amewataka pia watendaji wote wa TAMISEMI kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo.
“Sio mimi niliosema CCM imeoza” – RIDHIWANI KIKWETE
Kauli ya kwanza ya RPC Kagera baada ya Juma Nyosso kudaiwa kumpiga shabiki