Tumezoea kuona mtu akifanya kazi anapewa mshahara fedha sasa hii ni tofauti kidogo mtu wangu wa nguvu wafanyakazi katika kiwanda cha matofali kusini mashariki mwa China wanaokidai kiwanda hicho mishahara yao yenye thamani ya $14,050, wamelipwa matofali na kampuni hiyo.
Shirika la habari Xinhua, limesema takribani wafanyakazi 30 wa kiwanda hicho katika eneo Nanchang, katika jimbo la Jiangxi, wamekubali kulipwa matofali 290,000 badala ya mshahara wanaodai.
Gazeti la Jiangxi Daily limeripoti kuwa wafanyakazi hao, wote wakiwa ni wahamiaji, wametoka katika eneo la milima la jimbo la Yunnan Kusini Magharibi na hawakuwa na namna ili kuweza kuishi.
Baada ya chama chao cha wafanyakazi kuingilia kati na kwa msaada wa Mahakama, wafanyakazi hao walikubali kupokea matofali hayo kutoka wamiliki wa kiwanda hicho badala ya mshahara wao ambao hawajalipwa.
Xinhua limesema kuwa muajiri wao, ambaye hakutajwa jina katika vyombo vya habari, bado anajaribu kutafakari namna ya kuwalipa, deni la Yuan 10,000 ambazo bado wanamdai wafanyakazi hao.
BREAKING: RAIS MAGUFULI AMETENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI BUTIAMA