Leo January 23, 2018 Waandaji wa Tuzo za Oscar wametaja list ya waigizaji na filamu zinazowania tuzo hizo good news ni kwamba Filamu inayohusu shambulizi la kigaidi ambapo watu 28 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera +254 Kenya na kundi la Al-shabaab mwaka 2014 imeteuliwa kuwania tuzo hizo maarufu Duniani 2018.
Filamu hiyo ambayo ilikuwa imeshinda Tuzo za Oscar kitengo cha wanafunzi mwaka 2017 na kuwa filamu ya kwanza kutoka Kenya kushinda tuzo hiyo.
Filamu ya Watu Wote imetajwa kuwania kitengo cha Filamu Bora Fupi: Matukio Halisi. Itashindana na filamu nyingine nne ambazo ni “Dekalb Elementary”, “The Eleven O’Clock”, “My Nephew Emmett“ na “The Silent Child”.
Ni kwa mara ya kwanza ambapo filamu kutoka nchini kenya imeteuliwa kuwania tuzo ya Oscars. Mwandaaji wa filamu hiyo amesema Matrid Nyaga “Kenya sasa imepanda ngazi, tunaongoza katika kueleza ulimwengu hadithi za Afrika,”.
“Ni hadithi kuhusu Kenya na undugu wa Wakenya, inaonyesha njia mwafaka ya kukabiliana na ugaidi kote Ulimwenguni”.– Matrid Nyaga
VIDEO: BIASHARA KUJIONGEZA !! BAJAJI YA DAR YENYE FREE WI-FI