Serikali ya Ufilipino imeeleza kuwa wanategemea mlipuko mkubwa zaidi wa Volcano katika Mlima Mayon ambao ulianza kulipuka January 13, 2018 na kusababisha maelfu ya wakazi wa eneo hilo kuhamishwa makazi.
Mpaka kufikia asubuhi ya leo, Mamlaka zilikuwa zimeondoa watu waliokaribu na eneo la mlima kwa kilometa nane na kutenga eneo hilo ambalo lava hiyo inaweza kufikia ili kuepuka kuathiri watu.
Moshi wa Volcano hiyo hadi sasa umefikia kilometa kumi angani na tayari watu zaidi ya 40, 000 wameshatolewa eneo hilo huku shule zikifungwa na wito ukitolewa kwa raia kukaa ndani ya nyumba zao ili kuepuka madhara yanayoweza kutokana na volcano hiyo.
VIDEO: “Asanteni mliotuma video, tumewakamata madereva”
EXCLUSIVE :Kutumia bendera ya Taifa ni kosa kisheria
https://youtu.be/XigBe1IneJc