Ni habari kutoka Arusha Tanzania ambapo Afisa Tarafa wa Themi Felician Mtahengerwa amekuja kwenye headlines kwa habari ya kupiga marufuku Wanawake kwenda sokoni na watoto.
Felician amesema hii inawahusu Wanawake wote Wafanyabiashara >>> “Unakuta Mama anakaa sokoni na mtoto kuanzia saa kumi na moja alfajiri mpaka saa mbili usiku, ni marufuku kuanzia leo“
“Hatuamini kwamba Mama huyo atashindwa kupata Elfu 30 ya kumlipa Msichana wa kazi wa kubaki nyumbani na mtoto, atafute hata ndugu yake wa kufanya hiyo kazi“
January 23, 2018 Felician kwa kushirikiana na Kamati ya ulinzi na Usalama amekamata Watoto zaidi ya 100 ambao hawaendi Shule na badala yake wamekua wakifanya biashara katika masoko mbalimbali ya Arusha.
VIDEO: Nabii Tito amwambia Kamanda “mimi natumia Biblia” TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI