Taarifa zilizotufikia Ayo TV na millardayo.com leo January 24, 2018 ni kuhusu kifo cha Jaji Mstaafu Robert Kisanga ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency ya Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa John Kahyoza na Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu Thomas Mihayo kwa nyakati tofauti.
Jaji Kisanga kabla ya kustaafu mwaka 2008 amewahi kuwa Jaji kwenye Mahakama ya Rufaa nchini na amewahi kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pia amewahi kufanya kazi katika Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Marufuku kuanzia leo Mama kubeba Mtoto na kwenda nae sokoni Arusha
Sheria inasemaje kwa alichofanya Nabii Tito ???