Stori zinazomhusu Rais Donald Trump zinaendelea kushika headlines hasa barani Afrika ambapo taarifa iliyopo sasa ni kuwa atakutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa masuala ya kiuchumi World Economic Forum (WEF) unaofanyika mjini Davos, Uswizi.
Kagame atakuwa kiongozi wa pekee wa bara Afrika anayetarajiwa kukutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani H.R McMaster.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa unatokea kukiwa na malalamiko dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika kuwa ”machafu” au ya “mabwege” katika mkutano wa kuzungumzia sera za uhamiaji ambapo baadaye alikana madai hayo.
Mkutano wa rais Trump na Kagame, ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na Marekani na kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo Biashara na Usalama.
VIDEO: “ASANTENI MLIOTUMA VIDEO” TUMEWAKAMATA MADEREVA