Leo January 25, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba ametangaza rasmi kusimamisha zoezi la utoaji wa hati za kusafiria za jumla na kwa makundi mpaka pale watakapokuwa wameweka utaratibu wa kuendelea kufanya hivyo.
Dr. Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo na kusema hatua hiyo imekuja baada ya kupokea taarifa ya mateso wanayoyapata vijana wanaosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nje ya nchi kwa kisingizo cha kufanyakazi tofauti tofauti.
“Nasimamisha utoaji wa hati ya kusafiria ‘Passport’ za jumla za makundi za vijana wanaokuwa wanapata mikasa hiyo ya kunyanyaswa, kutumikishwa, kuteswa kikatili na wengine kuwekwa rehani kwa masuala ya dawa za kulevya”, -Dr. Mwigulu Nchemba.
BREAKING: SAID AMWAGA MACHOZI BAADA YA SCORPION KUHUKUMIWA MIAKA 7