Mwanaume mmoja nchini Uingereza anayejulikana kwa jina la Paul Playle, 43, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu jela baada ya kujifanya mpenzi wa zamani wa mkewe na kuanza kuwasiliana na mkewe huyo kama anamtaka warudiane kimapenzi kwa miaka miwili mfululizo.
Inaelezwa kuwa lengo la mwanaume huyo kufanya hivyo ilikuwa ni kumchunguza mkewe huyo kama bado anaweza kurudiana na mpenzi wake huyo wa zamani au hata kama anatamani kurudiana naye.
Wakati haya yote yakiendelea bado mwanaume huyo alijifanya kuwa mume mwema aliyemfariji mkewe, kila wakati mkewe alipomshtakia kuhusu usumbufu anaoupata kutoka kwa mpenziwe wa zamani ambaye hakujuwa kuwa ulikuwa ni mchezo wa mumewe.
Mwanamke huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya awali (nursery) ameeleza jinsi gani ameumizwa na kitendo hicho cha mumewe na kusema ameshafikiria hata kujiua kwani hafahamu jinsi gani suala hilo limeweza kutokea.
Akitoa hukumu hiyo Jaji Christine Henson ameeleza kuwa alichofanya mwanaume huyo ni kitendo cha kumdhalilisha mke wake tena ambaye ameishi naye kwenye ndoa kwa miaka 27 kwa sababu tu ya kuwa na wivu.
Waziri Mwigulu asimamisha zoezi la utoaji wa hati za kusafiria (Passport)
BILIONI 660 zimetolewa na Serikali kuboresha Jiji la Dar es salaam