.
Kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger amekiri kwamba angeweza kuchagua kutokumsaini Kim Kallstrom kama angekuwa na muda zaidi wa kufikiria kuhusu dili hilo.
Kallstrom, 31, alijiunga na Arsenal kwa mkopo katika masaa ya mwisho ya siku ya mwisho ya dirisha dogo la usajili akitokea Spartak Moscow akija kuziba pengo la majeruhi Aaron Ramsey na Mathieu Flamini aliyesimamishwa
Hata hivyo, imekuja kugundulika kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden ana matatizo ya maumivu ya mgongo ambayo yatamfanya akaei nje ya dimba mpaka mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza Wenger baada ya mchezo wa ushindi wa jana dhidi ya Crystal Palace, alisema: “Ilinijia kichwani tusikamilishe usajili ule na kama nisingemsajili kama kungekuwa na siku mbili au tatu za kuchagua mchezaji mwingine. Lakini lilikuwa limebakia lisaa limoja kabla ya dirisha kufungwa, hivyo nikaamua kumsajili Kallstrom.
“Alianza kupata maumivu ya mgongo siku mbili nyuma kabla hajawasili kwetu na wakati anafanyiwa vipimo ilionekana ana tatizo kidogo kwenye mgongo wake.
“Lakini watu wengi wenye tatizo kama lake wanakuwa hawatambui kama wana tatizo hilo, ni vigumu mno kumjua mchezaji mwenye tatizo hilo – hata hivyo klabu yake ya Spartak imekubali kulipa mshahara wake kwa wiki sita.” -Wenger