Moto umezuka kwenye hospitali moja huko Korea Kusini usiku wa kuamkia Ijumaa ya leo January 26, 2018 na kusababisha vifo zaidi ya watu 30 huku mamia ya wengine waliokuwa wakitibiwa hospitalini hapo wakijeruhiwa vibaya.
Moto huo ulizuka katika Hospitali ya Sejong iliyo katika Mji wa Miryang kipindi ambacho jumla ya watu 194 walikuwa wanatibiwa huku Wazee wakiwa 94. Madaktari wameeleza idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na wingi wa mejeruhi kwenye tukio hilo.
Korea Kusini imekuwa na matukio mengi ya moto ambayo husababisha vifo. Mwisho wa wiki iliyopita katika hoteli ya Seoul uliwaka moto ambao uliua watu sita, Polisi walifanikiwa kumkamata aliyeanzisha moto huo ambaye inadaiwa alianzisha moto huo baada ya kukataliwa kupewa chumba kwenye hoteli hiyo kwa kuwa alikuwa amelewa.
TRL inapoteza zaidi ya Mil.200 kwa siku kutokana na treni kutofanya kazi.
Serikali yatoa miezi 6 kwa wakazi wa Kilosa waliojirani na Reli kuhama