Mahakama nchini Niger imewahukumu wanajeshi 9 kifungo cha miaka mitano hadi 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya jaribio la kumpindua Rais wa nchi hiyo Mahamadou Issoufou miaka miwili iliyopita.
Hukumu hiyo ilisomwa siku ya jana January 26, 2018 na Jaji Ibrahim Daoudika ambapo alimhukumu kiongozi wa kikundi hicho ambaye pia alikuwa Jenerali wa Jeshi Salou Souleymane na wengine wawili miaka 15, huku wanajeshi wengine sita wakihukumiwa miaka 5 hadi 10.
Baada ya hukumu hiyo kusomwa, Mwanasheria wa upande wa utetezi Nabara Ycouba alieleza vyombo vya habari kuwa hawakutegemea kesi ingeisha jinsi ilivyoisha, lakini Mahakama ina uhuru na imesema wanajeshi hawa walipanga njama dhidi ya serikali.
“Sheria hairuhusu kukata rufaa kwa kosa hili, nitazungumza na wateja wangu kuona tunafanyaje” – Nabara Ycouba
Msemaji wa Jeshi la Polisi kaongelea ishu ya Nyalandu iliyotolewa Bungeni