Leo January 28, 2018 Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema upatikanaji wa haki Mahakamani sio lazima mtu ashinde kesi, bali haki bora ni ile inayopatikana kwa usuluhishi kuanzia nyumbani.
Jaji Mkuu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa wiki sheria, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja DSM ambapo amesema katika utoaji wa haki kuna changamoto nyingi ikiwemo vifaa na majengo.
Prof. Juma amesema watu wengi wanaokwenda Mahakamani wanaamini haki ni kushinda kesi tu bila kujua kama kuna mchakato.
“Sio lazima ukija Mahakamani ushinde kesi, kwani ili haki ipatikane kuna mchakato mrefu ambapo hata Mahakama inapoamua kukusikiliza hiyo ni moja ya hatua ya haki,”-Prof. Juma
Pia amesema jambo la msingi ili haki ipatikane mapema ni kusuluhishana, ambapo watu wanaweza kusuluhishana kuanzia nyumbani kabla ya kufika Mahakamani.
Prof. Juma pia amewataka wananchi wachukue hatua na waache kulalamika pindi wanapoona sheria imekiukwa, ili wananchi wawe na imani na Mahakama lazima watumishi wake wawe na maadili.
“Akawaambia mkiona Waziri anakuja Siha, Mkuu wa wilaya pasueni gari lake”-Dr Mollel