Unaambiwa shabiki mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Mbeya City iliyochezwa Februari 2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Shabiki huyu ambaye jina lake ni Matei Cosmas (28) ni mkazi wa eneo la Buza Njiapanda Kitunda Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe madai yakiwa ni kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchini.
Tff pia wametoa wito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa na kusema tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.
Source:Salehjembe.