Rais wa Marekani Donald Trump amemjibu Jay-Z baada ya mwanamuziki huyo wa Rap kumuita “mdudu hatari” na kumkemea kwa jinsi anavyowachukulia watu weusi.
Katika ukurasa wake wa Twitter Trump amesema kuwa “kiwango cha Wamarekani wasio na ajira kimeripotiwa kuwa cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa!” kwa sababu ya sera zake.
Wa-Marekani wenye asili ya Afrika wasio na ajira ni asilimia 6.8%, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi kutokea nchini humo.
Trump ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha Van Jones Show cha CNN, Jay-Z alisema kuwa ukiangalia viwango vya ukosefu wa ajira ni ” kukosa ufahamu wa mambo”.
“Sio suala la ukosefu wa pesa pekee lenye umuhimu … pesa hazileti furaha… hazileti. Hii ni kushindwa kuelewa ukweli. Uwachukulie watu kama binadamu …hilo ndio suala kuu la muhimu.”
Aidha amesema kuwa kuchaguliwa kwa Trump kulitokana na kushindwa kutatuliwa kwa masuala kadhaa.
Somebody please inform Jay-Z that because of my policies, Black Unemployment has just been reported to be at the LOWEST RATE EVER RECORDED!
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) January 28, 2018
“Inasikitisha na inaumiza, Kila mtu anahisi hasira. Baada ya hasira, inasikitisha sana kwa sababu ni kama ana dharau kwa watu wote .”- Jay Z
DAKIKA 8 ZA LOWASSA AKIMNADI MGOMBEA KINONDONI “HUYU BWANA ACHANA NAYE”