Leo January 29, 2018 Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amezindua kituo cha Mafunzo na Habari za Mahakama Kisutu ili kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama na wadau wa sheria.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo hicho, Jaji Mkuu Prof. Juma amesema kituo hicho kimejengwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) kikiwa na malengo kadhaa ikiwemo kuhakikisha haki inawafikia wananchi na walengwa kwa urahisi zaidi.
Pia amesema TEHAMA inarahisisha kazi kwa sababu kutoa haki kwa kutumia TEHAMA wanawafikia wananchi wengi kwa urahisi zaidi.
Prof. Juma amesema kuna maeneo mapya kabisa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na watumishi wa Mahakama ambayo ni Makosa ya Mtandao, Makosa yanayotokana na miamala ya simu na Dawa za kulevya
Amesema Mahakimu na waendesha mashtaka wakipata mafunzo hayo watakuwa na uelewa mmoja katika kutoa haki.
Amesema kwa sasa wanapata taarifa kutoka kisutu lakini bado hawajaweza kupata taarifa katika Mahakama zote hivyo watumishi wa Mahakama wawasaidie kukusanya taarifa hizo.
MFUMO MPYA WA TEHAMA KUANZA KUTUMIKA MAHAKAMANI
Ulipitwa na hii? RC Gambo katangaza kuwasimamisha kazi na kutoa barua ya onyo