Taarifa za mchana huu January 29, 2018 ni kwamba basi la Kampuni ya Tahmeed linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha limeteketea kwa moto mida ya saa 6:30 mchana eneo la Kitumbi.
Ayo TV na millardayo.com imezungumza na kondakta wa basi hilo ambaye amekataa kutaja jina lake ambaye amethibitisha tukio hilo, hata hivyo ameeleza kuwa hakuna vifo wala abiria yeyote kujeruhiwa.
Ameeleza kuwa basi limeteketea lote, na hadi sasa chanzo cha moto bado hakijajulikana na mpaka muda huu wanasubiri wanaohusika kuchukua gari hilo kufika eneo hilo na kulichukua.
“Moto ulianza tu kuwaka ndani ya gari, ndipo dereva alipolisimamisha na abiria wakaanza kushuka, abiria wote walifanikiwa kutoka bila kudhurika kabisa.” – Kondakta Tahmeed Bus
TILIONI 2.6 zitajenga Reli ya umeme ‘Standard Gauge’ toka DSM mpaka Morogoro