Viongozi wakuu wa Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wametangaza kuwa maandalizi yamekamilika kuelekea kumuapisha kiongozi wake Raila Odinga kama rais wa watu leo January 30, 2018 katika bustani ya uhuru jijini Nairobi.
Mkurugenzi Mkuu wa NASA Norman Magaya amewaambia wafuasi wa NASA kukusanyika katika uwanja wa Uhuru Park kwa maandalizi ya kumuapisha Odinga na Naibu wake Kalonzo Musyoka saa nne asubuhi.
Wasiwasi umetokea kuhusu iwapo shughuli hiyo itafanyika katika bustani hiyo baada ya jeshi la Polisi kupiga marufuku mkusanyiko wa watu katika bustani hiyo.
Kamanda wa jiji la Nairobi Japhet Koome, amesema hataruhusu yeyote kuonekana katika bustani hiyo.“Siwezi kuruhusu watu kwenda kuumizana katika bustani ya Uhuru Park,”.
ILICHOKIBAINI BODI YA MIKOPO BAADA KUFANYA UKAGUZI SHULE YA GREEN ACRES