Nchi 23 za Africa zimesaini makubaliano ya soko huria la usafiri wa anga lengo kuu likiwa kukuza uchumi wa nchi hizo kwa kuongeza mwingiliano, kupunguza gharama za usafiri wa anga ikizingatiwa kuwa Afrika inatajwa kuwa bara linaloongoza kwa gharama za juu za usafiri huo.
Viongozi wa nchi hizo ikiwemo Afrika Kusini, Nigeria na Kenya wamekubaliana kuwa mfumo huu utafungua milango kwa ndege za nchi hizo kuweza kuruka kwenye anga la nchi wanachama wa makubaliano hayo.
Taarifa za taasisi ya kimataifa ya usafiri wa anga ya Umoja wa Mataifa ya (International Civil Aviation Organisation) inaonesha kuwa idadi ya watu wote Afrika inachukua 15% ya idadi ya watu wote Duniani lakini wanaotumia usafiri wa anga ni 3% tu.
“Barani Afrika usafiri wa anga unachukuliwa kama suala la anasa wakati Amerika na Ulaya mtu yeyote anaweza kwenda popote kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa wiki, hiki ndicho tunachokihitaji Afrika.” – David Kajange, Mkuu wa kitengo cha Usafiri na Utalii wa Umoja wa Afrika
Zitto Kabwe ataja viongozi ambao atawateua ikitokea amekuwa Rais wa TZ