Leo January 30, 2018 Benki ya Taifa ya Kenya imetangaza kupunguza wafanyakazi 150 wakieleza kuwa nia ya kufanya zoezi hilo ni kupunguza gharama za kujiendesha.
Benki hiyo imejipanga kupunguza wafanyakazi wenye miaka zaidi ya 35 na ambao wamefanya kazi zaidi ya miaka 5 na kuruhusiwa kuchukua mafao yao mapema kwa hiari.
Inaelezwa kuwa hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu kwa Benki hii kupunguza wafanyakazi wengi ambapo mwaka 2014 ilipunguza wafanyakazi 200.
Hatahivyo uongozi wa benki hiyo umeamua kuongeza kiwango cha fedha kitakachotolewa kutokana na wao kuachishwa kazi kwa wafanyakazi ambao wana miaka zaidi ya 50. Benki itawalipa mshahara wa miezi miwili kwa mwaka mzima, kwa miaka inayobakia wao kutimiza umri wa kustaafu ambao ni miaka 60.
“Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 7 kutoka Mwaka Jana” Dr. Msonde