Rais John Magufuli leo January 31, 2018 amezindua Hati mpya za Kusafiria za Kielektroniki mjini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo ameongea mambo makubwa 12 kuhusiana na hati hizo na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ujumla.
"Passport ya nchi hii tumekuwa nayo kwa kipindi kirefu sana, mfumo uliotumika kuitengeneza ni wa kizamani, na haukuwekewa usalama wa kutosha, hii ndio sababu ya baadhi ya watu kuweza kughushi." Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Passport tunayoizindua leo ina alama nyingi za usalama, hii itasaidia kupunguza kama si kuondoa kabisa uwezekano wa kughushiwa, zaidi ya hapo, baadhi ya taarifa zake zitakuwa zinasomeka kwenye mifumo ya kielektroniki bila kulazimika kuipeleka yenyewe." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Passport hii ya kielektroniki itaathiria kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa uhamiaji mtandao yaani e-migration, ambao umepangwa kutekelezwa kwa awamu nne." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Awamu ya pili baada ya hii ya passport ya kielektroniki itahusu kufunga mfumo wa visa yaani e-visa pamoja na hati za ukaaji, awamu ya tatu itakuwa ya usimamizi wa mipaka kwa njia ya kielektronic yaani e-boarder management system." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Awamu ya nne itahusu kupanua huduma za uhamiaji mtandao kwenye ofisi za balozi zetu pamoja na wilaya zenye shughuli nyingi za uhamiaji." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani Mil 57.82 sawa na Tsh Bilioni 127.2 lakini awali ulipangwa kutekelezwa kwa Dola Milioni 226 ambayo ni sawa na Tsh Bilioni 400, walipanga kutupiga kwenye pesa za Watanzania." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Dr Makakala katafute eneo, nitawapa Tshs Bilioni 10, wakati wowote mtakapozihitaji muanze kujenga Makao Makuu ya Uhamiaji, na ninatoa hizi kama shukrani kwa kazi kubwa unayofanya wewe na watendaji wako." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Juzi wameingia wahamiaji zaidi ya 1500 kutoka DRC, lakini walioripoti kambi ya wakimbizi ninaambiwa ni chini ya 1000, wengine wameshaingia mitaani, ni jukumu lenu kuwasaka popote." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
'Ifike mahali anaposhikwa mhamiaji haramu, na kuulizwa taarifa zake za mikoa aliyopitia, wachukuliwe hatua Wakuu wote wa Uhamiaji wa mikoa hiyo yote ili waanze kujifunza majukumu yao ya kufanya kazi." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Zoezi la Idara ya Uhamiaji la kutambua watu wasio raia nchini liwe endelevu ili kuwatambua wanaoishi nchini bila vibali, wanaofanya kazi bila vibali vya kazi, na wanaofanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Mfumo huu wa kielektroniki pia utategemeea uadilifu na utendaji kazi wa watumishi wa idara hii, bado wako watumishi wa idara hii ambao hawataki kubadilika, wanaendelea kuendekeza vitendo vya rushwa, watu hawa ni wachache lakini wanaichafua sana idara hii." – Rais John Magufui
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
"Kamishna Mkuu wachukulieni hatua watu hawa, ikibidi wafukuzeni, wapo Watanzania wengi wazalendo wanaotafuta kazi, najua hili watu wa Uhamiaji hawawezi kushangilia kwasababu hakuna anayetaka kufukuzwa basi muache rushwa ili msiendelee kufukuzwa." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) January 31, 2018
LIVE: JPM akihutubia kwenye Uzinduzi wa Hati ya kusafiria ya Kielektroniki
‘Wako ambao tumewakamata wakiwafanyia wengine mitihani’ Dr. Msonde