Club ya Arsenal ya England leo imetangaza rasmi kufanikiwa kumsajili nahodha wa timu ya taifa ya Gabon aliyekuwa anaichezea club ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang.
Jezi namba atakayovaa Aubameyang itatangazwa baadae lakini kwa sasa Arsenal wametangaza kumsajili staa huyo wa Gabon mwenye umri wa miaka 28 kwa dau la pound milioni 56, kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu na atakuwa akilipwa pound 180,000 kwa wiki.
Kwa sasa Aubameyang ndio mchezaji ghali katika kikosi cha Arsenal baada ya Alexandre Lacazette aliyesajili kwa pound milioni 52 lakini ndio mchezaji pekee wa taifa la Gabon kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika 2015.
Aubameyang anatajwa kama moja kati ya washambuliaji bora duniani, akiwa na Borussia Dortmund katika Ligi Kuu Ujerumani akicheza game 144 amefunga jumla ya magoli 98 lakini amefunga jumla ya magoli 172 katika michezo 213 akiwa na Dortmund katika michezo yote.
Manara baada ya Yanga kupata penati “Baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu”