Leo January 31, 2018 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametembelea Wilaya ya Nyamagana kuongea na wakazi wa Buhongwa wenye migogoro ya ardhi pamoja na kukabidhi hati za nyumba na viwanja 3,000.
“Serikali imegundua katika Miji yetu mingi, wananchi wanaishi katika makazi holela, ni wachache wanaoishi katika makazi rasmi, maeneo mnayokaa hayakupimwa, mimi nawapongeza mliojitokeza leo 3000, hati ni uwezeshaji, ukiwa na hati mtapata mikopo, mliopata hati kuanzia leo ni matajiri,”– Waziri Lukuvi
JPM AKIHUTUBIA KWENYE UZINDUZI WA HATI YA KUSAFIRIA YA KIELEKTRONIKI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA