Moja kati ya stori zilizowashitua wengi katika upande wa soka ni baada ya taarifa kudaiwa kuvuja kuwa club ya West Ham United ya England haitaki kusajili wachezaji wa kiafrika, kitu ambacho kimetafsiriwa na baadhi ya watu kama ubaguzi wa rangi.
Mtandao wa DailyMail baada ya kuzinasa taarifa hizo ulimtafuta mkurugenzi wa michezo anayesimamia masuala ya usajili Tony Henry na kukiri kuwa wameamua kutosajili wachezaji zaidi wa kiafrika na kuwa West Ham inataka kudhibiti idadi ya wachezaji wa kiafrika kwenye timu yao.
Sababu za West Ham kutohitaji wachezaji wa kiafrika wamesema kuwa “Wana tabia mbaya pale wanapokuwa hawapo katika timu wanasababisha ghasia na sio ubaguzi wa rangi wakati mwingine wana tabia mbaya”
Taarifa zimetolewa ufafanuzi baada ya kuvuja kwenye magazeti kwa barua aliyokuwa ametumiwa wakala ikimpa kigezo cha kutowatafutia wachezaji kutokea Afrika, kwa sasa West Ham United ina wachezaji saba raia kutokea bara la Afrika.
Manara baada ya Yanga kupata penati “Baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu”