Kenya bado inaendelea kuzishika headlines na stori nayo kusogezea leo February 1, 2018 ni kuhusu vituo vya TV vilivyofungwa na Serikali ambapo Mahakama Kuu jijini Nairobi, imeagiza serikali kuwasha mitambo ya Television tatu zilizofungiwa baada ya kudaiwa kuwa na mpango wa kurusha LIVE kuapishwa kwa kiongozi wa NASA Raila Odinga, kuwa rais wa watu.
Kesi hiyo iliwasilishwa Mahakamani na Mwanaharakati Okiya Omtatah ambaye ameiambia Mahakama kuwa, serikali imekwenda kinyume na Katiba inayoruhusu haki ya wananchi kupata habari kupitia vyombo hivyo.
Agizo hili limekuja baada shinikizo pia kutoka kwa Mashirika ya kiraia na yale ya haki za binadamu kutoka ndani na nje ya nchi hiyo kulaani kitendo hicho.
Mashirika hayo yakiongozwa na Amnesty International, yamesema kitendo hicho kinatishia Uhuru wa vyombo vya Habari nchini humo na kinarudisha nyuma juhudi za demokrasia.
Houghton Irungu, Mkuu wa Amnesty International nchini Kenya ameongeza kuwa kitendo hicho ni cha aibu na kinayumbisha pia uchumi wa Taifa hilo.
LIVE: CHADEMA WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.