Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Kilimanjaro imewafikisha Mahakamani watuhumiwa wawili na kuwasomewa mashtaka nane. Mtuhumiwa wa kwanza ni mlinzi wa Uhamiaji Hassan Idd Muna aliyeshawishi na kupokea rushwa kwa raia wa India ili waweze kumwezesha raia huyo kupata hati ya kusafiria.
Mwingine aliyefikishwa mahakamani ni aliyejifanya Mkuu wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu Rajabu Mandally ambaye akishirikiana na mlinzi huyo wa uhamiaji alishawishi kupata elfu kumi na nane na baadae kupokea shilingi elfu ishirini.
Wakili wa TAKUKURU Suzan Kimaro amesema wakiwa wawili walishawishi kupata shilingi laki sita na kupunguziana hadi kufikia shilingi laki nne na baadae kupokea shilingi laki mbili.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Aidan Mwinakwa amewaachia kwa dhamana kwa masharti yakuwa na mdhamini mmoja atakayesaini fungu la dhamana la shilingi milioni 3 kila mmoja kesi itatajwa tena February 18 mwaka huu.
CHADEMA WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.