Leo ni siku ya tano ya mwezi wa pili kwa mwaka 2014 na unaweza kuchukua dakika chache kujua vitu hivi kuhusu leo pamoja na vitu vingine ambavyo vinaweza kuwa ni vipya kwako.
Kama ulikua hujui leo ni birthday ya wakali kusakata soka Cristiano Ronaldo,Carlos Tevez,Adnan Januzaj,Neymar wote pamoja wamezaliwa tarehe 5/2 lakini miaka tofauti.
Cristiano Ronaldo amezaliwa mwaka 1985 na leo anatimiza miaka 29,Carlos Tevez amezaliwa mwaka 1984 anatimiza miaka 30 ,Neymar amezaliwa mwaka 1992 ambapo leo anafikisha mika 22,Adnan Januzaj kutoka Manchester united anatimiza mika 19 ambapo amezaliwa mwaka 1995.
Umewai kusikia kuhusu Saadani National Park, hii ni mbuga ambayo wanyama huwa wanaenda kukaa(ku-chil) pembeni ya beach kwasababu mbuga hii ipo karibu na bahari ya hindi.
“Where bush meet beach” ndiyo sentensi maarufu inayoitambulisha Saadani kwa utofauti wake wa kipekee ambapo watalii wanaweza kuwa kwenye boti na kuona wanyama waliopo kandokando ya beach. Usijiulize ipo wapi kwasababu ipo hapahapa nyumbani Tanzania
Umewahi kumsikia mtu anaitwa Leonardo Da Vinci ambaye anatajwa kuwa ni mchoraji,mbunifu wa majengo(Architect),Mwanahisabati (Mathematician), Mwanamuziki, Engineer, Inventor, Mwanajiolojia (Geologist),Cartographer,mwandishi na vingine vingi.
Da Vinci amepata umaarufu kwa kuchora picha za Monalisa,The last supper,Vitruvian Man na Lady with an Ermine.
Da Vinci anatajwa kuwa ni mmoja kati ya watu waliowai kufanya vitu vingi kwenye field ya art na science na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa .