Nikusogezee stori kutoka kwa Majirani zetu Kenya kwa President Uhuru Kenyatta ambapo wakazi wa eneo la hifadhi ya Arabuko Sokoke wamefanikiwa kuachana kabisa na shughuli za kukata misitu baada ya kugundua fursa kubwa inayowaingizia kipato kutoka katika msitu huo.
Fursa hii ni ya ‘kilimo cha vipepeo’ ambapo inaelezwa kuwa katika hifadhi hiyo kuna utajiri mkubwa sana wa vipepeo jambo ambalo wakazi wa eneo hilo walipoambiwa inaweza kuwa rufsa ya kibiashara wakaanza kuitumia na sasa inawalipa.
Wanakijiji hao sasa wanachukua vipepeo hao na kuwasafirisha nje ya nchi kwa biashara. Siku za nyuma walipokuwa wakifanya ukataji miti haramu walikuwa wakipata Dola za Marekani 150 kwa wiki sawa na Tsh 360,000 au pungufu.
Inaelezwa kuwa kwa sasa wanapata takribani Dola 200 kwa wiki sawa na Tshs 480,000. Wakulima hao wa vipepeo wamefundishwa aina za vipepeo zinazohitajika zaidi sokoni. Inaripotiwa kuwa kwenye msitu huo kuna aina za vipepeo zaidi ya 263.
“Kauli zetu zinaweza zisiifurahishe Serikali, hili ni tatizo kubwa” –Hussein Bashe
Maamuzi ya Serikali kwa Wauguzi wanaowanyanyasa wajawazito