Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana na wito kwa vijana kujiajiri ni agenda zinazozungumzwa sana nchini na watu wa nyadhifa, taaluma na rika mbalimbali.
Ayo TV na millardayo.com zimefanya mahojiano na kijana Makoye Philbert ambaye ni maarufu jijini Dar es Salaam kwa biashara yake ya kuuza juice zijulikanazo kama ‘Mak Juice’ ambaye ameeleza jinsi gani alianza biashara hiyo.
Mjasiriamali huyu ameeleza kuwa alipanga kujiajiri wakati bado akiwa ameajiriwa na hata alikuwa tayari kuanza biashara hiyo alianza kwa mtaji wa Tsh 7000, lakini sasa biashara hiyo imeajiri vijana wa Kitanzania wengi ikiwa bei ya juice hiyo hiyo imebaki kuwa Tshs 2000 kama biashara hiyo ilivyoanza.
Mlemavu wa macho aliyebuni nguo za Viongozi nchini
Kauli ya Jeshi la Polisi Kagera baada Mgombea Udiwani aliyepotea kupatikana