Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa leo February 6, 2018 amezungumza mambo mbalimbali katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV alipokuwa akifanyiwa mahojiano ikiwa ni pamoja na maamuzi yake ya kujiondoa kwenye chama hicho.
Dr. Slaa ameeleza kuwa alijiuzulu usiku ule ule ambao Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alikwenda kwenye Kamati Kuu ya CHADEMA, ambapo asubuhi ya siku hiyo alikaa kikao na viongozi wanne toka saa 3 hadi saa 9 na akakataa uamuzi huo wa kumpokea Lowassa.
Pia wakaingia kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama ambapo walibishana hadi saa 12 jioni lakini bado alikataa suala hilo lakini pia alikataa hata baada ya kuundwa kamati nyingine ya kumshawishi kukubali uamuzi huo, lakini pia hakukubali na hivyo baadae akaandika barua mbili za kujiuzulu.
“Kwenye Demokrasia lazima wengi uwape, kama hamuwezi kukubaliana unachagua kuuungana nao au kuachana nao.” Dr Slaa
Dr Slaa ameeleza kuwa alifikia uamuzi huo wa kujiuzulu na kuondoka kwenye chama kwani siku zote chama hicho kilikuwa kwenye vita dhidi ya mafisadi lakini chama kikageuka, hiyo ni sawa na ‘choo kuhamia chumbani’.
MAKJUICE: KAANZA NA MTAJI WA ELFU 7 MPAKA DALADALA YA KUUZA JUICE MTAANI