Leo February 6, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu raia wa Uganda, Winfred Businge (33) aliyekamatwa na zaidi ya TSh.Bilioni 2 katika Airport ya JNIA DSM kulipa faini ya TSh.Milioni 100 ama kwenda jela miaka 3 baada ya kukiri kosa la kukamatwa na fedha hizo alizoshindwa kuzitolea maelezo.
Businge alikwepa adhabu ya kwenda jela na kuachiwa huru baada ya kufanikiwa kulipa faini ya hiyo ya TSh.Milioni 100.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa huyo kukiri kosa.
Hakimu Shaidi alisema kutokana na mshtakiwa kukiri kosa, Mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 3 ama kulipa faini ya Sh.milioni 100, pia fedha alizokamatwa nazo atarudishiwa.
Katika kesi hiyo, Businhe ambaye ni Kalani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, anadaiwa alitenda kosa hilo December 11, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Inadaiwa akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam alikutwa ameingia nchini akiwa na USD Milioni 1 (zaidi ya Sh.Bil 2) ambazo alishindwa kuzitolea maelezo kwa wakala wa forodha.
MKAPA, JK, LOWASSA, MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WALIVYOUAGA MWILI WA KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA