Stori ninayokusogezea leo February 6. 2018 ni kumhusu John Tshibangu, Kanali aliyeasi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amefikishwa nchini humo na kuzuiliwa kusikojulikana nchini humo, baada ya kukamtawa nchini Tanzania.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasa ya Kongo imethibitisha kumpokea Kanali John Tshibangu aliyekamatwa na vyombo vya usalama vya Tanzania wiki moja iliyopita baada ya kuonekana kwenye mkanda wa video akimpa siku 45 rais Joseph Kabila awe amejiuzulu au aipindue Serikali yake.
Waziri wa Sheria nchini DRC Alexis Tambwe Mwamba amethibitisha kusafirishwa nchini humo kwa kanali Tshibangu na kusisitiza kuwa kesi yake itasikilizwa kwa uwazi kama zilivyo kesi nyingine akithibitisha kuwa atashtakiwa kwa makosa ya uhaini.
January 19, 2018 Kanali John Tshibangu aliasi na kutangaza vita dhidi ya Rais Kabila, huku akiimpa siku 45 aachie madaraka.
MKAPA, JK, LOWASSA, MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WALIVYOUAGA MWILI WA KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA