Mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hilaly ni miongoni mwa Wabunge waliosimama Bungeni akichangia mapendekezo yake katika taarifa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na taarifa ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2017 ambapo alilalamikia hatua za Serikali kuwanyima uhuru wafanyabiashara wa mazao kwa kuwazuia kusafirisha nje ya nchi bila kuwa na vibali maalum na kusababisha kutengeneza mazingira ya rushwa.
Aeshi amesema ..>>>“Waziri amesema wameruhusu kusafirisha mahindi kokote lakini hapohapo anaweka kikwazo kingine cha kuwa na kibali, hapo ni kutengeneza rushwa. Nasikitika sana tunapochangia mawaziri wanacheka”
Kauli ya Prof Tibaijuka kuhusu Diwani CHADEMA aliyedaiwa kutekwa