Nakusogezea stori kutoka mkoani Arusha ambapo Leo February 7, 2018 Waziri wa mambo ya ndani nchini, DR Mwigulu Nchemba ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya hekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mwigulu akishirikiana na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha,(RPC) Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapo walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo Mwigulu amesema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi.
Akizungumza na askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini aliwambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza dawa ya kulevya zinazolimwa mashambani lakini waongeze juhudi pia katika kupambana na dawa ya kulevya zinazotengenezwa viwandani.
BREAKING: “WAMECHUKULIWA WATU KUTOKA ZANZIBAR WAMELETWA KINONDONI” CHADEMA