Ni kawaida kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kukuletea bei mpya za Mafuta nchini kila Jumatano ya kwanza ya mwezi na leo February 7, 2018 imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikiongezeka.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ambapo amesema bei za rejareja zimeongezeka kwa Petroli ikiwa ni Tsh59 sawa na asilimia 2.70, Dizeli Tsh46 (sawa na asilimia 2.30), na mafuta ya taa kwa Tsh24 (sawa na asilimia 1.17).
Amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambazo kwa Petroli ni Tsh58.57 sawa na asilimia 2.85, Dizeli kwa Tsh46.48 (sawa na asilimia 2.44) na mafuta ya taa kwa Tsh23.75 (sawa na asilimia 1.24).
“Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Januari 3. Bei za mafuta ya taa hazijabadilika kwa sababu hakuna yaliyoingizwa nchini kupitia bandari hiyo Januari,” -Mchany.
“Ongezeko la bei za mafuta ya petroli na dizeli katika Mkoa wa Tanga linatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji,” -Mchany.
BREAKING: “WAMECHUKULIWA WATU KUTOKA ZANZIBAR WAMELETWA KINONDONI” CHADEMA