Nakusogezea stori kutoka mkoani Arusha ambapo February 7, 2018 Waziri wa mambo ya ndani nchini, DR Mwigulu Nchemba ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya hekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mwigulu akishirikiana na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha,(RPC) Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapo walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.
TOP 10: HIZI NDIZO HOTELI ZENYE VYUMBA VYA BEI ZA JUU ZAIDI DUNIANI