Waziri Mkuu wa Australia Malcolm Turnbull ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo itaomba msamaha kwa waathirika wote nchini humo kwa waliofanyika unyanyasaji wa kingono walipokuwa watoto.
Uamuzi na ahadi hii ya Turnbull unakuja baada ya kuhitimishwa kwa uchunguzi wa miaka minne ambao umegundua kuwa maelfu ya watoto miaka iliyopita wamefanyiwa unyanyasaji kwenye taasisi mbalimbali za nchini Australia.
Unyanyasaji huu unaripotiwa kufanyika katika maeneo ya mashuleni, kwenye makanisa, klabu za michezo na maeneo mengineyo. Tume iliyofanya uchunguzi huo ilitoa mapendekezo 400 ikiwa ni pamoja na kuomba Kanisa Katoliki kutengeneza upya kanuni zake za kutofanya tendo la ndoa kabla ya ndoa.
BREAKING: Diamond Platnumz alivyofika Mahakamani Kisutu leo
Wema Sepetu alivyofika Mahakamani Kisutu na Wakili Msando