Katika hali ya kushangaza, wanafunzi wa chuo wamegoma kufuata mapendekezo yaliyotolewa na uongozi wa chuo hicho ya kutovaa nguo fupi kwa madai kuwa zinawakwaza baadhi ya wanafunzi wenzao na waalimu katika taasisi hiyo nchini Columbia.
Kutokana na mapendekezo hayo yaliyoandikwa kwenye tovuti ya chuo hicho January 30, 2018 wanafunzi wameungana na kusema suala hilo ni la kuendekeza ubaguzi hivyo wakaamua kuanzisha kampeni ya kushawishi watu wote, wanaume na wanawake kuvaa nguo fupi siku ya February 8, 2018.
Wanafunzi wa Chuo hicho Kikuu cha Medellín’s Pontifical Bolivarian wameeleza kuwa mapendekezo hayo yalilenga moja kwa moja kuwakandamiza wanawake wa chuo hicho kwa kuhusisha wanavyovaa na matendo ya ngono, jambo ambalo wamedai ndilo wanalolipinga.
Baada ya hayo kutokea chuo hicho kimetoa taarifa rasmi kuzungumzia suala hilo na kusema kuwa chuo hicho kinaheshimu utu na mgawanyiko wa tabia za watu (personalities) na hakijawahi kupangia wanafunzi nini cha kuvaa hivyo hayo yalikuwa ni mapendekezo hususani kwa wanafunzi wapya.
MAONI YA WANANCHI: ‘Vitu tunavyohitaji kwa atakayeshinda Ubunge Kinondoni’
Roma, Stamina na Madee wametajwa na Meya kuikaribisha timu ya KMC