Staa wa zamani wa club za Arsenal na Man United Robin van Persie amerudi kwenye headlines nyumbani kwao Uholanzi baada ya kurudi katika timu yake ya Feyenoord kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 toka alipoondoka mwaka 2004 na kujiunga na Arsenal.
Robin van Persie amerudi Feyernoord mwaka huu 2018 akitokea Fenerbahce ya Uturuki na usiku wa jana amefanikiwa kuifungia Feyernoord goli lake la kwanza ikiwa ni baada ya miaka 14 toka alipofanya hivyo mara ya mwisho 2004, Van Persie aliifungia Feyernoord goli la tatu katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya FC Groningen.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Robin van Persie alijipatia umaarufu mkubwa akiwa katika club ya Arsenal ya England aliyoichezea kwa miaka nane kabla ya mwaka 2012 kuamua kujiunga na Man United aliyodumu nayo kwa miaka mitatu na baadae akajiunga na Fenerbahce aliyodumu nayo kwa miaka mitatu pia.
https://youtu.be/tvEEnNH6368
Simba imetangaza kumpeleka Haruna Niyonzima India